Tuesday, April 26, 2005

ZOEZI

WEWE NI MWANAUME NA YEYE NI MTOTO MDOGO
MIMI NI MTU NA YEYE NI MNYAMA MDOGO
KITI KIDOGO NA MWALIMU MFUPI
RAFIKI YANGU NI MPISHI MZURI NA KIATU CHAKE NI KIKUBWA
MGENI NI MWANAMKE MREMBO NA MWENYEJI NI KIPOFU

METHALI ZA KISWAHILI

Nenda hapa ujifunze methali za kiswahili na tafsiri zake.

MAANDISHI YA KWENYE KANGA

Bonyeza hapa ujifunze misamiati mipya kwa kupitia maandishi ya kwenye kanga.

NABII ALIPOMTEMBELEA RAFIKI YAKE

Nabii: Hodiiii
Jumanne: Karibu. Wewe nani?
Nabii: Asante. Mimi Nabii
Jumanne: Nabii? Nabii ni nani?
Nabii: Umenisahau? Tulikutana ufukweni wiki iliyopita
Jumanne: Ah, nimekumbuka. Nakuja kufungua mlango

Mlango unafunguliwa.

Jumanne: Karibu ndani
Nabii: Asante sana. Nimepita kukusalimu. Habari za toka siku ile?
Jumanne: Nzuri tu. Joto sana siku hizi.
Nabii: Kweli kabisa. Kuna joto sana.
Jumanne: karibu chai.
Nabii: Asante, nimeshakula.
Jumanne: Kunywa kidogo. Huwezi kuondoka bila kula chochote. Ngoja nikanunue chapati maana najua unapenda sana chapati.
Nabii: Chai kikombe kimoja na chapati moja vitanitosha.

Jumanne anakwenda gengeni kwa Bi. Sharifa. Anarudi na chapati mbili. Anaandaa chai. Wanakunywa chai na chapati huku wakiongea masuala ya soka, siasa, mapenzi, na muziki. Baada ya kuongea kwa kama dakika arobaini na tano, Nabii anaaga.

Nabii: Asante sana mshikaji kwa chai na chapati. Ninakwenda nyumbani. Tutaonana tena siku nyingine.
Jumanne: Karibu tena. Kama unakwenda ufukweni mwisho wa wiki niambie twende wote

***********************************************************************************

Monday, April 25, 2005

SHAIRI: WALIOZALIWA

Waliozaliwa
Kila kitu tayari! Msitarini!
Moja, mbili, tatu! Kimbia! Hima!
Wakati ni mfupi na hakuna aliyeshinda.
- Euphrates Kezilahabi (Karibu Ndani. 1988)

Thursday, April 21, 2005

SOMO LA TAREHE KUMI NA TISA

Niliwaahidi kuwa nitaweka hapa kwenye blogu somo la jumanne iliyopita. Bonyeza hapa.

MIMI, WEWE, YEYE, WAO, SISI, NINYI

Mimi ni mwalimu
Wewe ni mwanafuzi
Yeye ni mwanaume
Wao ni watoto
Sisi ni binadamu
Ninyi ni Wamarekani

Tuesday, April 19, 2005

WIKIPEDIA YA KISWAHILI

Bonyeza/Kongoli hapa uone Wikipedia ya Kiswahili.

SASA NI SAA NGAPI?

Sasa ni saa ngapi?
Sasa ni saa moja kamili (7:oo)
Sasa ni saa mbili na dakika kumi (8:10)
Sasa ni saa saba na dakika kumi na tano/ Sasa ni saa saba na robo (1:15)
Sasa ni saa kumi na nusu/ Sasa ni saa kumi na dakika thelathini (4:30)
Sasa ni saa tatu kasorobo/ Sasa ni saa mbili na dakika 45 (8:43)
Sasa ni saa nane na dakika thelathini na tano/ Sasa ni saa tisa kasoro dakika ishirini na tano (2:35)
*************************************************

Utakuja darasani saa ngapi?
Utaamka saa ngapi?
Ulikula saa ngapi?

NINAJIPENDA, NINAMPENDA....

Ninajipenda = mimi
Ninampenda = yeye
Ninawapenda = wao
Ninakupenda = wewe
Ninawapenda = ninyi
Tunajipenda = sisi

Tuesday, April 05, 2005

KUMBUKA! KUMBUKA! KUMBUKA!

Darasa = Darasani
Shule = Shuleni
Nyumba = Nyumbani
Kanisa = Kanisani
Hoteli = Hotelini
Duka = Dukani
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Ninauliza = Ninajiuliza
Ninatazama = Ninajitazama
Ninapenda = Ninajipenda

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Unasemaje.....?
Unaandikaje.....?
Unaulizaje.....?
Unakwendaje....?

Monday, April 04, 2005

FURAHA ANAKUTANA NA TUMAINI

Furaha: Habari Tumaini?
Tumaini: Nzuri. Mambo?
Furaha: Poa. Unakwenda wapi?
Tumaini: Ninakwenda darasani. Nimetoka maktaba kusoma. Na wewe unakwenda wapi?
Furaha: Ninakwenda kula. Nilikuwa nimelala. Sasa ninasikia njaa
Tumaini: Mimi nitakula baadaye nikitoka darasani. Unakula nini leo?
Furaha: Nitakula wali na kuku, maji, na papai
Tumaini: Haya, kwaheri tutaonana baadaye kwenye darasa la Kiswahili
Furaha: Kwaheri. Masomo mema.

LIKIZO YA KIPUPWE

Utasemaje "spring break?"

Utasema: 1. Likizo ya kipupwe
2. Likizo ya msimu (season) wa kipupwe

Sunday, April 03, 2005

WIMBO

Hujambo,
Hujambo rafiki,
Habari gani,
Nzuri sana x 2

Marekani nchi yetu,
Hakuna matata....