KWENDA KWA HOSPITALI/ KWA DAKITARI
Nia: Shimakoo dakitari
Dakitari: Marahaba, habari
Nia: Nzuri kiasi, najisikia mgonjwa
Dakitari: unaumwa nini?
Nia: Ninaumwa kichwa na tumbo. Viungo mwilini vinauma na sina nguvu kabisa
Dakitari: Toka lini?
Nia: Toka juzi usiku
Dakitari: Umetumia dawa yoyote?
Nia: Ndio, nimekula panado kupunguza maumivu
Dakitari: Je unaweza kula chakula
Nia: Sina hamu ya kula kabisa. Nikila ninatapika
Dakitari: Je una....
Kabla Dakitari hajamaliza kuuliza Nia ananyanyuka.
Nia: Tafadhali naomba kwenda kujisaidia. Choo kiko wapi?
Dakitari: Choo cha wanawake kiko mlango wa pili, upande wa kushoto.
Nia anaondoka haraka haraka kwenda chooni. Anarudi baada ya dakika kumi.
Dakitari: Unapata haja vizuri?
Nia: Hapana, ninaendesha
Dakitari: Basi utakwenda maabara ukapime damu halafu utaniletea majibu.
Nia anakwenda kupima damu. Baada ya muda anarudi kwa Dakitari na majibu ya damu. Dakitari anasoma majibu kwa makini.
Dakitari: Naona una malaria. Nitakuandikia dawa ya malaria na nyingine ya kuendesha. Utatumia mara tatu kwa siku. Rudi hospitali siku ya jumanne asubuhi saa tatu. Ugua pole
Nia: Asante

2 Comments:
This comment has been removed by a blog administrator.
This comment has been removed by a blog administrator.
Post a Comment
<< Home