NABII ALIPOMTEMBELEA RAFIKI YAKE
Nabii: Hodiiii
Jumanne: Karibu. Wewe nani?
Nabii: Asante. Mimi Nabii
Jumanne: Nabii? Nabii ni nani?
Nabii: Umenisahau? Tulikutana ufukweni wiki iliyopita
Jumanne: Ah, nimekumbuka. Nakuja kufungua mlango
Mlango unafunguliwa.
Jumanne: Karibu ndani
Nabii: Asante sana. Nimepita kukusalimu. Habari za toka siku ile?
Jumanne: Nzuri tu. Joto sana siku hizi.
Nabii: Kweli kabisa. Kuna joto sana.
Jumanne: karibu chai.
Nabii: Asante, nimeshakula.
Jumanne: Kunywa kidogo. Huwezi kuondoka bila kula chochote. Ngoja nikanunue chapati maana najua unapenda sana chapati.
Nabii: Chai kikombe kimoja na chapati moja vitanitosha.
Jumanne anakwenda gengeni kwa Bi. Sharifa. Anarudi na chapati mbili. Anaandaa chai. Wanakunywa chai na chapati huku wakiongea masuala ya soka, siasa, mapenzi, na muziki. Baada ya kuongea kwa kama dakika arobaini na tano, Nabii anaaga.
Nabii: Asante sana mshikaji kwa chai na chapati. Ninakwenda nyumbani. Tutaonana tena siku nyingine.
Jumanne: Karibu tena. Kama unakwenda ufukweni mwisho wa wiki niambie twende wote
***********************************************************************************

0 Comments:
Post a Comment
<< Home