MRADI WA KISWAHILI MOMBASA
Nawashukuru Nia na Haki walionipatia kiungo cha habari kuhusu mradi wa Kiswahili mjini Mombasa, Kenya. Nenda
KARIBUNI KWENYE UKUMBI WA KISWAHILI
Nawashukuru Nia na Haki walionipatia kiungo cha habari kuhusu mradi wa Kiswahili mjini Mombasa, Kenya. Nenda
Wanataaluma wengi sasa wanaanza kutumia blogu katika kazi zao na mambo yao binafsi. Bonyeza hapa.
BILA
CHINI
JUU
NDANI
NJE
ILA
HATA
BADO
HALAFU/KISHA
LABDA
MAANA/KWASABABU/SABABU
HIVI
VILE
VILEVILE
PIA
KATIKA
Furaha: Naomba nionyeshe njia ya kwenda kwa fundi cherehani
Masanja: Fundi cherehani yupi?
Furaha: Unamkumbuka fundi cherehani aliyeshona gauni langu la krisimasi?
Masanja: Aah, panda basi la kwenda Kariakoo, shuka kituo cha Magomeni. Vuka barabara. Nenda upande wa pili. Utaona muuza madafu mkono wa kushoto, nenda moja kwa moja hadi utakapoona duka la madawa upande wa kulia. Chukua barabara ya mkono wa kushoto, nenda hadi utakapokuta njia panda. Ukifika hapo njia panda uliza mtu yeyote kwa fundi Mgonja.
Furaha anaandika maelezo yote kisha anamshukuru Masanja na wanaagana.
Jua linachomoza kila alfajiri toka upande wa mashariki
Jua linazama alasiri upande wa magharibi
Antaktika iko ncha ya kaskazini ya dunia
Kuna baridi kali sana katika ncha ya kusini ya dunia
Amani na Nabii wanaongea kwenye simu ya mkono.
Amani: Uko wapi?
Nabii: Nipo posta
Amani: Tumaini yuko wapi?
Nabii: Sijui. Labda yumo benki
** -ko: indefinite location
-po: definite location
-mo: refers to location inside
"KI":
1. Nikienda Tanzania nitapanda mlima Kilimanjaro
2. Kila nikila maharagwe ninajisikia kulala
"PO":
1. Nilipokwenda Tanzania nilipanda mlima Kilimanjaro
2. Kila nilipokula maharagwe nilijisikia kulala
M-WA
Umoja: Ambaye: mtoto niliyemtaja anakuja
Wingi: Ambao: watu niliowaona wanatoka Marekani
M-MI
Umoja: Ambao: mti ulioanguka ni mrefu sana
Wingi: Ambayo: miti iliyoanguka ni mirefu sana
KI-VI
Umoja: Ambacho: Kisu kilichonikata ni cheusi
Wingi: Ambavyo: Visu vilivyonikata ni vyeusi
Nia: Shimakoo dakitari
Dakitari: Marahaba, habari
Nia: Nzuri kiasi, najisikia mgonjwa
Dakitari: unaumwa nini?
Nia: Ninaumwa kichwa na tumbo. Viungo mwilini vinauma na sina nguvu kabisa
Dakitari: Toka lini?
Nia: Toka juzi usiku
Dakitari: Umetumia dawa yoyote?
Nia: Ndio, nimekula panado kupunguza maumivu
Dakitari: Je unaweza kula chakula
Nia: Sina hamu ya kula kabisa. Nikila ninatapika
Dakitari: Je una....
Kabla Dakitari hajamaliza kuuliza Nia ananyanyuka.
Nia: Tafadhali naomba kwenda kujisaidia. Choo kiko wapi?
Dakitari: Choo cha wanawake kiko mlango wa pili, upande wa kushoto.
Nia anaondoka haraka haraka kwenda chooni. Anarudi baada ya dakika kumi.
Dakitari: Unapata haja vizuri?
Nia: Hapana, ninaendesha
Dakitari: Basi utakwenda maabara ukapime damu halafu utaniletea majibu.
Nia anakwenda kupima damu. Baada ya muda anarudi kwa Dakitari na majibu ya damu. Dakitari anasoma majibu kwa makini.
Dakitari: Naona una malaria. Nitakuandikia dawa ya malaria na nyingine ya kuendesha. Utatumia mara tatu kwa siku. Rudi hospitali siku ya jumanne asubuhi saa tatu. Ugua pole
Nia: Asante
Soma insha hii ya kiingereza iliyoandikwa na Mukolozi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kuhusu Kiswahili kama lugha ya kitaifa na kimataifa. Hapa.
WEWE NI MWANAUME NA YEYE NI MTOTO MDOGO
MIMI NI MTU NA YEYE NI MNYAMA MDOGO
KITI KIDOGO NA MWALIMU MFUPI
RAFIKI YANGU NI MPISHI MZURI NA KIATU CHAKE NI KIKUBWA
MGENI NI MWANAMKE MREMBO NA MWENYEJI NI KIPOFU
Bonyeza hapa ujifunze misamiati mipya kwa kupitia maandishi ya kwenye kanga.
Nabii: Hodiiii
Jumanne: Karibu. Wewe nani?
Nabii: Asante. Mimi Nabii
Jumanne: Nabii? Nabii ni nani?
Nabii: Umenisahau? Tulikutana ufukweni wiki iliyopita
Jumanne: Ah, nimekumbuka. Nakuja kufungua mlango
Mlango unafunguliwa.
Jumanne: Karibu ndani
Nabii: Asante sana. Nimepita kukusalimu. Habari za toka siku ile?
Jumanne: Nzuri tu. Joto sana siku hizi.
Nabii: Kweli kabisa. Kuna joto sana.
Jumanne: karibu chai.
Nabii: Asante, nimeshakula.
Jumanne: Kunywa kidogo. Huwezi kuondoka bila kula chochote. Ngoja nikanunue chapati maana najua unapenda sana chapati.
Nabii: Chai kikombe kimoja na chapati moja vitanitosha.
Jumanne anakwenda gengeni kwa Bi. Sharifa. Anarudi na chapati mbili. Anaandaa chai. Wanakunywa chai na chapati huku wakiongea masuala ya soka, siasa, mapenzi, na muziki. Baada ya kuongea kwa kama dakika arobaini na tano, Nabii anaaga.
Nabii: Asante sana mshikaji kwa chai na chapati. Ninakwenda nyumbani. Tutaonana tena siku nyingine.
Jumanne: Karibu tena. Kama unakwenda ufukweni mwisho wa wiki niambie twende wote
***********************************************************************************
Niliwaahidi kuwa nitaweka hapa kwenye blogu somo la jumanne iliyopita. Bonyeza hapa.